Ubalozi uliendelea kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchini zilizopo katika eneo la uwakilishi ikiwemo Jamaica, Colombia, Chile, Guyana kwa Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel J. Nchimbi kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa viongozi wa Kitaifa wa nchi hizo katika nyakati tofati. Katika mazungumzo na viongozi wa nchi hizo, walikubaliana kuendeleza ushirikiano wa nyanja mbalimbali zikiwemo vita dhidi ya madawa ya kulevya, sekta ya gesi na mafuta, uvuvi, Maliasili na utalii hususan uhifadhi wa mbuga za Wanyama.